Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salim Kijuu (kulia)
akimshukuru Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL)
Kamugisha Kazaura (kushoto) mara baada ya kupokea msaada wa mifuko 600
ya saruji ambayo ni sawa na tani 30 yenye thamani ya Sh. milioni 10.
Wafanyakazi na Uongozi wa Shirika
la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wametoa msaada wa Sh. milioni
20 kusaidia kununua vifaa vya ujenzi kwa waathirika wa tetemekola ardhi
mkoani Kagera.
Akikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa
Mkoa wa huo Meja Jenerali Mstaafu Salim Kijuu, Mwenyekiti wa Bodi ya
TPDC Balozi Dkt. Ben Moses amefafanua kuwa msaada huo unalenga
kuwasaidia kununua mabati na saruji kwa waathirika wa tetemeko hilo
lililoukumba mkoa huo.
“Sisi TPDC tunatoa msaada wetu
kama sehemu ya Watanzania na tatizo hili ni letu sote na Watanzania ni
wamoja” alisema Dkt. Moses.
Kwa upande wake Meja Jenerali
Mstaafu Kijuu amewashukuru TPDC kwa mchango wao na kubainisha kuwa
hakuna kitu kidogo katika kutoa na kuwahakikishia wadau wote wanaotoa
michango yao kuwa misaada hyote inayotolewa itatumika kwa malengo
yaliyokusudiwa na itasaidia kuwarudishia makazi waathirika wa tetemeko
hilo.
Aidha, Mkuu huyo wa mkoa
amewataka watu wote wenye mapenzi mema kuendelee kuwachangia waathirika
wa tetemeko hilo na waige mifano ya watu na taasisi mbalimbali
wanaoendelea kutoa misaada kwa mkoa wa Kagera ili kuwarudishia makazi
wananchi walioathirika maafa hayo.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi
wa TPDC Kapuulya Musomba amesema kuwa huo sio mwisho wao katika
kuchangia waathirika wa tetemeko la ardhi, bali wanaendelea
kuwahamasisha wadau wa mafuta na gesi yakiwemo makampuni ya ndani na nje
ya nchi ili kuwafanya wananchi waweze kuendelea na kazi zao za kila
siku kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla.
Wakati huo huo Kampuni ya Simu
Tanzania (TTCL) nao wametoa msaada wa mifuko saruji 600 ambayo ni sawa
na tani 30 yenye thamani ya Sh. milioni 10 ikiwa ni mchango wa wa
kampuni hiyo katika kuwashika mkono na kuwafuta machozi wananchi wa
Kagera.
0 comments:
Post a Comment