Mwanaume 1 kati ya 3 wana matatizo ya nguvu za kiume – hii ni kulingana
na utafiti uliofanyika. Upungufu wa nguvu za kiume unasababishwa na
mambo mengi ikiwemo ukosefu wa virutubisho muhimu mwilini. Ni jambo
linaloweza kupata ufumbuzi kwa urahisi kama utazingatia kula vizuri na
kufanya mazoezi.
Ili kuongeza stamina kwenye mapenzi si lazima kutumia madawa makali kama
viagra au vilevi vikali. Madawa na pombe hukupa nguvu zinazoisha kwa
muda mfupi, lakini hukuletea madhara makubwa yatakayokuandama kwa muda
mrefu zaidi. Ili kupata suluhishi la uhakika ni vizuri kuzingatia
vyakula vinavyoweza kukuongezea stamina na kujenga mwili wako vizuri na
kukupa uwezo wa kufanya mapenzi vizuri zaidi bila kutumia "booster". Vyakula ni suluhishi maridhawa na asilia kwenye kila kitu maishani mwako.
Sababu za kukosa nguvu za kiume
Ili kutatua tatizo ni muhimu kung’oa kabisa mzizi wake. Mwili wako una
maarifa ya kujirekebisha pasipo kuhitaji vilevi au mawada, unachotakiwa
kuzingatia ni chakula bora tu. Wahenga walisema, utakuwa bora kama chakula unachokula. Je wewe unakula chakula bora ili kulinda heshima yako nyumbani?
Vitu vinavyoweza kupelekea kupungua kwa nguvu za kiume ni kama:
- Kutokuwa na mzunguko mzuri wa damu mwilini, hasa sehemu za viungo vya uzazi kwa mwanaume.
- Kutokuwa na kiwango cha kutosha cha homoni ya Testosterone
- Kupungukiwa protini na hivyo kukosa amino asidi mwilini
Jinsi ya kuongeza nguvu za kiume
Leo napenda tuangalie vyakula ambavyo vinasaidia kuboresha nguvu za
kiume na kusaidia kwa kiasi kikubwa kudumisha mapenzi na kulinda
mahusiano na ndoa.
1. Blueberry
Blueberry ni matunda yanayosaidia sana kuongeza nguvu za kiume, wengi
hupendelea kuyaita ‘viagra’ asilia kutokana na kazi inayoifanya mwilini.
Blueberries ina virutubishi vinavyoimarisha mishipa ya damu na kusaidia
mzunguko mzuri wa damu mwilini. Damu ndio kila kitu katika nguvu za
kiume.
Vilevile, blueberries zina nyuzinyuzi (fiber)
ambazo husaidia kuondoa kolesteroli (Cholestrol) mwilini kabla
hazijanganda kwenye mishipa ya damu. Kuwa na mzunguko mzuri wa damu
husaidia mwanaume aweze kuhimiri mapenzi wa muda mrefu zaidi.
2. Mtini (Figs)
Mtini (figs) ni matunda yenye kiwango kikubwa cha amino asidi, ambayo ni
kiungo kikubwa katika kuzalisha homoni mwilini. Homoni ndio kishawishi
cha nguvu za kiume mwilini. Kukosa amino asidi huweza kusababisha kukosa
hamu ya mapenzi au kupungukiwa na nguvu za kiume.
3. Chaza/Kombe wabichi (Raw Oysters)
Chaza wana kiwango kikubwa cha madini ya zinc. Madini za zinc hutumika katika utengenezaji wa homoni ya testosterone, shahawa na mbegu za kiume.
Uwingi wa uzalishwaji wa testosterone mwilini huathiri pia hamu ya
mapenzi na nguvu za kiume – ikiwa kidogo huondoa hamu, ikiwa nyingi
hupelekea hamu na nguvu zaidi.
Kupungukiwa kwa madini ya zinc husababisha kupungua kwa nguvu za kiume,
udhaifu (uhanithi), na kushuka kwa kiwango cha uwezo wa kufanya mapenzi.
4. Karanga
Karanga ni chanzo kikubwa cha kujenga protini mwilini. Karanga huwa na
kiwango kikubwa cha amino asidi ambayo husaidia kuweka vizuri mfumo wa
damu, hivyo kusababisha kuongezeka kwa kiwango cha ufanyaji mapenzi.
5. Vitunguu saumu
Kitunguu saumu kina allicin, kiambato kinachosaidia mzunguko mzuri wa
damu kwenye viungo vya uzazi. Kuwa na mzunguko mzuri wa damu kwenye uume
ni sababu kubwa ya kuongeza stamina ya kufanya mapenzi.
6. Ndizi
Kuwa na stamina ni muhimu katika ufanyaji mapenzi. Ndizi ni chanzo
kikubwa cha vitamin B ambayo husaidia sana katika kuongeza stamina na
nguvu mwilini hasa wakati wa kufanya kazi nzito. Ndizi ina kimeng’enyo
cha Bromelain ambacho huongeza nguvu za kiume, ashki ya mapenzi (libido).
7. Chocolate
Chocolate inasaidia kuongeza stamina kwenye kufanya mapenzi kwasababu ina viambato vya phenylethylamine na alkaloid.
Phenylethylamine ni kiambato kinachopelekea kujisikia vizuri, hasa
wakati wa kufanya mapenzi na alkaloid huongeza stamina na nguvu wakati
wa mapenzi.
Vyakula ni bora kuliko madawa makali
Mie
binafsi nashauri kutumia njia asilia katika kutatua matatizo yako yote
ya kiafya. Mwili una njia zake za kurekebisha kila kitu. Ukiona kuna
tatizo inaashiria kuna upungufu ambao unatakiwa kurekebishwa. Kutumia
madawa makali hudhoofisha mwili na hivyo kuupunguzia uwezo wa kufanya
kazi kama inavyotakiwa. Ni vizuri kama utamuona daktari kama ukiona
hakuna kinachowezekana kabla hujaanza kutumia madawa.
Mara
nyingi njia asilia hutumia muda mrefu sana kuleta mabadiliko, lakini
matokeo yake hudumu zaidi kuliko kutumia madawa makali ambayo hutibua
mfumo wa kawaida wa ufanyaji kazi wa mwili wako. Mie nashauri uangalie
jinsi unavyokula, nenda kapime vizuri. Kama jogoo ameshindwa kupanda
mtungi, ruksa kuangalia njia mbadala.
Ni
vizuri kula kwa kiasi kabla ya kufanya mapenzi, hasa wakati wa usiku
kabla ya kwenda kulala. Kuvimbiwa husababisha mwili kufanya kazi ya
ziada ya kumeng’enya chakula hivyo kuingiwa na uchovu, uvivu na
kunyong’onyea. Hii husabisha kukosa usingizi na kupungua kwa umahiri
wako katika kufanya shughuli nyingi zinazohitaji nguvu, ikiwemo mapenzi,
kwa ufasaha. Usije kumtafuta mchawi wakati wewe ndio unajiroga, kuwa
makini.
Kama
ilivyo ada kwenye mambo mengi ya kiafya, hakuna muarobaini. Ni vizuri
ukajaribu kubadilisha chakula unachokula, fanya mazoezi mara kwa mara
ili kupata mwili wenye nguvu. Kama utakuwa na swali, weka maoni hapo
chini nasi tutakujibu bila kusika hukusu njia zaidi za kutatua tatizo la
nguvu za kiume.
0 comments:
Post a Comment