TANGOZO

TANGOZO
Latest News
Tuesday, June 28, 2016

SUGE KNIGHT AMSHITAKI CHRIS BROWN MAHAKAMANI

Suge Knight anamshtaki mwanamuzki mwenza wa R& B Chris Brown mahakamani pamoja na mmiliki wa kilabu moja ya usiku nchini Marekani kufuatia ufyatulianaji wa risasi uliotokea katika kilabu hiyo mwaka 2014.

Mwanamuziki huyo wa zamani alipigwa risasi mara saba katika hafla ya Chris Brown.
Kesi hiyo iliowasilishwa katika mahakama ya Los Angeles inamshtaki Chris Brown na kilabu ya West Hollywood Ckub 1 Oak kwa kushindwa kuweka usalama wa kutosha na kumruhusu mtu mmoja aliyejihami kuingia katika kilabu hiyo.

Suge Knight alipigwa risasi tumboni,kifuani na mkono wa kushoto.
Kwa sasa Suge Knight anakabiliwa na kesi ya mauaji baada ya kumgonga mtu na kutoroka.
Inadaiwa kile kilichotokea katika kisa hicho ndio sababu ya yeye kufanya vitendo kama hivyo.
 
Alishtakiwa kwa kuwakanyaga watu wawili na kumuua mmoja huku mwengine akijeruhiwa vibaya.
Wakili wake anasema kuwa alikuwa akijaribu kuwatoroka washambuliaji .

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: SUGE KNIGHT AMSHITAKI CHRIS BROWN MAHAKAMANI Rating: 5 Reviewed By: SIMAMA BUKOBA