TANGOZO

TANGOZO
Latest News
Monday, September 19, 2016

Ndege ya Air Tanzania kuingia Dar wiki hii.

Moja kati ya ndege mbili zilizonunuliwa na serikali kuimarisha usafiri wa anga nchini, inatarajiwa kuwasili Jumanne wiki ijayo.

Kauli hiyo imetolewa na naibu spika wa bunge, Dk Tulia Ackson, wakati akitoa taarifa ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Pro Makame Mbarawa.

“Waziri Mbarawa ameniarifu kuwa, ndege hiyo itatua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere “,alisema Dk Tulia.

“Pia natoa wito kwa wabunge na viongozi kushiriki kuipokea ndege hiyo aina ya Dash 8-Q400 yenye uwezo wa kubeba abiria 76,”aliongeza.

Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli, imedhamiria kurejesha fahari ya sekta hiyo nchini kwa kuchukua hatua kadhaa, ikiwamo ya kununua ndege na kuboresha viwanja vya ndege nchini. Lengo ni kuhakikisha kuwa kila mkoa unakuwa na kiwanja cha ndege cha kisasa, chenye ubora unaofaa kutua ndege.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: Ndege ya Air Tanzania kuingia Dar wiki hii. Rating: 5 Reviewed By: SIMAMA BUKOBA