Makamu wa Rais, Mhe. Samia
Suluhu Hassan akimjulia hali mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika taasisi
ya saratani ya Ocean Road Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake
aliyoifanya katika hospitali hiyo leo Ijumaa (Julai 29, 2016).
(PICHA NA ISMAIL NGAYONGA- MAELEZO)
…………………………………………………………………………………………….
Na Beatrice Lyimo- MAELEZO
MAKAMU wa
Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya ziara yake ya kwanza katika
Hospitali ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Jijini Dar es Salaam kwa
lengo la kuona wagonjwa sambamba na kuangalia maendeleo ya hospital
hiyo.
Akiwa katika
ziara hiyo Mhe. Samia amebaini baadhi ya changamoto zinazoikabili
hospitali hiyo ikiwemo ya upungufu wa wauguzi na madaktari, uhaba wa
mashine za mionzi, upungufu wa vifaa tiba pamoja na upatikanaji wa dawa
za Saratani kwa wagonjwa hao.
Amesema kuwa
Serikali itahakikisha inaongeza mashine mbili mpya za mionzi kwa ajili
ya kupimia wagonjwa wanaosumbuliwa na matatizo ya Saratani na kuahidi
kupunguza deni la MSD wanaloidai hospital hiyo ili wagonjwa waweze
kupata dawa kwa gharama nafuu.
Mganga Mkuu
wa Hospitali hiyo Dk. Damian Msemo ameiomba Serikali kuwekeza bajeti ya
kutoshakatika hospital hiyo kwani inatoa huduma bure kwa wagonjwa
wanaosumbuliwa na matatizo hayo ambapo matibabu yake haa kwa upande wa
mashine ya mionzi hutumia gharama kubwa
Akifafanua
utaratibu wa kutibu wagonjwa wanaofika hospitalini hapo kutibiwa amesema
kuwa hospitali hiyo imeweka utaratibu mzuri wa kuwahudumia wagonjwa hao
ambapo mgonjwa anayefika mapema ndiye anayehudumiwa na kuongeza kuwa huwa wanatimu wagonjwa 160 kwa siku kuanzia asubuhi hadi usiku licha ya uhaba wa vifaa tiba walionao”
“Hospitali hii tumeweka utaratibu mzuri wa kuwahudumia wagonjwa wanaofika, mgonjwa anayefika mapema ndiye anayehudumiwa kwanza
ukiacha wagonjwa wa dharula” Amesema Dk. Msemo.
Amesema
wagonjwa wanaowafikia kutibiwa hospitalini hapo ni wengi ikilinganishwa
na vifaa tiba walivyonanvyo na kuwataka wananchi kuwa wavumilivu pale
wanapokumbana na changamoto mbalimbali.
Kwa upende
wao baadhi ya wagonjwa waliofika hospitalini hapo kupata matibabu
wameushukuru uongozi wa Hospitali ya Taasisi hiyo kwa kujituma mbali na
uhaba wa waauguzi na changamoto za upatikanaji wa mashine za mionzi na
dawa kwa ajili ya kutibu matatizo hayo
0 comments:
Post a Comment