TANGOZO

TANGOZO
Latest News
Saturday, July 16, 2016

MESEJI NZURI ZA MAPENZI KWA UMPENDAYE KWA DHATI

  1. Kuna miezi 12 katika mwaka…siku 30 katika mwezi…siku 7 katika wiki, masaa 24 katika siku…dakika 60 katika saa……lakini wewe ni mmoja tu maishani mwangu.
  2. Kuna vitu viwili zinavyoniamsha asubuhi na mapema: Alamu ya saa yangu na wewe
  3. Bongo zenye fikra kali huwa na mawazo, suluhu na sababu; ubongo wa kisayansi huwa na kanuni, nadharia na takwimu; wangu una wewe tu!
  4. Penzi linaweza kuelezewa kwa namna nyingi. Namna moja niijuayo nikumtumia mapenzi hayo mtu asomaye meseji hii.
  5. Kama ningeweza kubadili herufi, ningeweka yangu na yako kuwa pamoja.
  6. Umewekwa usiku ili tuweze tuukubali mchana, huzuni ili tuikubali furaha, ubaya ili tuukubali uzuri, wewe ili niyakunali mapenzi.
  7. Unaonekana kung’ara leo nilijuaje…….ni kwasababu unaonekana hivyo kila siku
  8. Mapenzi ni nini? Wale wasiopenda huita majukumu, wale wanaoyachezea huita mchezo, wale wasiokuwa nayo huita ndoto, na wale wanaoelewa huyaita mwisho wa safari, na mimi, mwisho wangu ni wewe.
  9. Kama mapenzi huweza kukimbiwa kwa kufumba macho yetu tu, basi nisingefunika macho kabisa. Sitaki sekunde ipite bila kukupenda wewe.
  10. Nilikuwa nikifiria kwamba ndoto haziwezi kuwa kweli, lakini nilibadili mawazo yangu pale tu nilipokuona wewe.
  11. Baadhi ya watu huzaliwa na vipaji. Huweza kufanya mambo mazuri kwa ujuzi wao, lakini hamna anayekufikia wewe, kwani ukinisogelea tu kila kitu huwa kizuri.
  12. Mwanamke ni yule amfanyaye mwanamme auhisi uanaume wake, wewe ni mwanamke mwenye sifa hizo.
  13. Kukusahau wewe ni ngumu lakini kunisahau mimi ni juu yako. Usinisahau kamwe, unaweza kuisahau meseji hii, lakini si mtumaji.
  14. Mambo yanapokwenda mrama kumbuka kuwa kuna Mungu peponi anayekupenda na kukuangalia, lakini yupo duniani anayekujali ambaye ni mimi peke yangu.
  15. Simu huboa wakati mwingine, kwani ni lazima ufungue meseji na kuzisoma, kuichaji simu kila mara, lakini usichoke kwani ndiyo inayotuwezesha tuwasiliane





























































.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: MESEJI NZURI ZA MAPENZI KWA UMPENDAYE KWA DHATI Rating: 5 Reviewed By: SIMAMA BUKOBA