Wanasema kama una bandama basi huwezi kujizuia kucheka popote pale
ulipo, hata kama ni kwenye eneo ambao hutakiwi uonyeshe tabasamu.
Kama ni hivyo basi huwezi kushangaa pale ambapo mkongwe katika filamu
za Kibongo, Abdallah Mkumbila ‘Muhogo Mchungu’ alipovunjwa mbavu na
mmoja ya waumini ndani ya msikiti wakati ibada ikiendelea katika kile
kipengele cha kutoa sadaka.
Akibonga na Juma3tata, Muhogo Mchungu anasema kila inapokaribia
sikukuu kubwa huwa kuna sadaka inatolewa kwa waumini mbalimbali katika
msikiti huo, ili kuwasaidia ambao wapo vibaya kiuchumi waweze kufurahia
sikukuu kama watu wengine.
“Kuna sadaka huwa inatolewa kila inapokaribia sikukuu na safari hii
kila muumini alipewa shilingi laki moja, sasa mimi nilijikuta naachia
kicheko pale nilipomuona muumini mmoja ambaye alikuwa kwenye swala
akiivuta ile hela aliyowekewa pembeni yake kwa hofu ya jirani yake
kumwibia.
“Unajua mtu akiwa kwenye swala, huwezi kumkatisha hivyo yule
aliyekuwa anazigawa zile laki moja moja baada ya kuona jamaa yupo kwenye
swala akaamua kumuwekea pembeni ili atakapomaliza kuswali aichukue.
Kweli pesa ni hatari, mtu hadi anafikia kuacha swala kwanza achukue
pesa? Ilinishangaza sana kwakweli,” anasema Muhogo Mchungu.
Muhogo Mchungu aliongeza: “Nilijiuliza, inamaana huyu jamaa hakufumba
macho? Hata kama yalikuwa wazi, aliwezaje kuona kilichokuwa kikiendelea
na kuachana na swala kisha akazisogeza zile fedha kwanza? Kila
nikikumbuka kwakweli nachoka kabisa.”
0 comments:
Post a Comment