TANGOZO

TANGOZO
Latest News
Wednesday, July 20, 2016

MZOGA WA NYANGUMI WA TANI 22 WENYEJI WA SHINDWA KUUBEBA

Wakaazi wa California Marekani wamelazimika kuvumilia uvundo kutoka baharini kwa zaidi ya majuma matatu baada ya mzoga wa nyangumi mkubwa kusombwa na maji hadi ufukweni.

Mnyama huyo mkubwa wa baharini anakisiwa kuwa na uzani wa takriban tani 22.

Hakuna kifaa chochote kilichokuwa na uwezo wa kuhamisha mzoga huo.
 angu juni tarehe 30 alipopatikana ameaga ,Wally mwenye urefu wa mita 14 alionekana akielea baharini karibu na ufukwe wa Los Angeles.

Nyangumi huyo wa kike, alianza kuvunda na kusababishia wakaazi wa maeneo karibu na bahari wasijue la kufanya kutokana na ukubwa wake.

Wenyeji waliwaajiri wafanyikazi wa mijengo ambao walikuwa na trekta kubwakubwa za kunyanyua mawe na misumeno ya moto.
Walimkata kata katika vipande vitatu lakini hata hivyo vilikuwa vizito mno kwa trekta za ujenzi.

Mwishowe waliagiza trekta kubwa zaidi yenye uwezo wa kunyanyua tani 10 ya mzoga huo unaovunda na kuibwaga baharini.

Wenyeji bado wanapata harufu mbaya majumbani mwao lakini wanaona kheri ikiwa mbali .
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: MZOGA WA NYANGUMI WA TANI 22 WENYEJI WA SHINDWA KUUBEBA Rating: 5 Reviewed By: SIMAMA BUKOBA