TANGOZO

TANGOZO
Latest News
Thursday, July 14, 2016

TANZANIA KUCHUANA NA IVORY COAST SOKA LA UFUKWENI

Timu ya Mpira wa Miguu Ufukweni ya Tanzania imepangwa kucheza na Ivory Coast kati ya Agosti 26, 27 au 28, 2016 kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mwaka 2017 zitakazofanyika Lagos, Nigeria.

Mchezo wa marudiano unatarajiwa kufanyika kati ya Septemba 16, 17, au 18.

Fainali za Mpira wa Miguu Ufukweni ambazo zitafahamika pia kama 2016 CAF Beach Soccer Championship, zitafanyika kuanzia Desemba 13 hadi 18, 2016 jijini Lagos, Nigeria kwa kushirikisha timu nane.

Tayari Nigeria imepasishwa kuwa mshiriki kwa sifa ya uenyeji wake. Timu nyingine 14 zinawania kucheza fainali hizo.

Timu nyingine zinazowania ni Cape Verde v Senegal, Uganda v Misri, Liberia v Morocco, Kenya v Ghana, Msumbiji v Madagascar, Sudan v Libya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: TANZANIA KUCHUANA NA IVORY COAST SOKA LA UFUKWENI Rating: 5 Reviewed By: SIMAMA BUKOBA