TANGOZO

TANGOZO
Latest News
Saturday, August 27, 2016

KALA JAREMIAH: NIMESHAOMBWA SANA NA WAZEE NIGOMBEE UBUNGE LIKINI NIMEKATAA KWASABABU MUDA BADO

Star wa Hip Hop Bongo anayetamba na wimbo wake wa ‘Wana Ndoto’, Kala Jeremiah amesema muda bado kwa yeye kujiingiza kwenye siasa na kugombea Ubunge japo kuwa ameshaombwa sana na wazee agombee na kuwa kiongozi wa Watanzania.

Akizungumza kupitia kipindi cha Hatua Tatu cha Times Fm asubuhi hii, Kala amedai anaogopa kuwa Mbunge wa Jimbo moja amabalo atalitazama zaidi na kuwasahau Watanzania wa maeneo mengine.

“Nimeshaombwa sana na Wazee, sana na wakina mama, na jamii inataka nigombee Ubunge, lakini mimi kwa sasa bado, unajua nikiwa Mbunge nitakuwa najihusisha na jimbo moja tu nitawasahau Watanzania wengine.

“Japo nitaendelea kukataa lakini itafika muda nitakubali maana wazee bado wataendelea kuniomba kwa hiyo nitakuwa sina jinsi” Amesema.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: KALA JAREMIAH: NIMESHAOMBWA SANA NA WAZEE NIGOMBEE UBUNGE LIKINI NIMEKATAA KWASABABU MUDA BADO Rating: 5 Reviewed By: SIMAMA BUKOBA