Manny Pacquiao
Bondia Manny Pacquiao ambaye pia ni Seneta nchini Ufilipino
anatarajia kurejea ulingoni Novemba 5 mwaka huu kwa pambano dhidi ya
mbabe aliyewahi kupigwa mara moja tu katika mapambano yake 28, Jessie
Vargas.
Meneja wa Manny Pacquiao, Koncz amesema kuwa wamejadiliana na Manny
Pacquiao na kuamua kumchagua bondia huyo huku akieleza kuwa wamemuacaha
Terrence Crawford ambaye watu wengi walikuwa wanampendekeza kutokana na
mtindo anaoutumia.
“Sipendi mtindo anaoutumia Crawford. Siamini kama ni mtindo unaomfaa Manny,” Koncz aliwaambia waandishi wa habari.
Alipoulizwa kama anachohofia ni kasi na namna anavyojilinda bondia huyo, alisema kuwa ni mtindo wake kwa ujumla akiwa jukwaani.
Hivi karibuni, Manny alikanusha tetesi za kurejea jukwaani mwaka huu
huku mkufunzi wake pia akidai angependa kama Manny angerudi ulingoni
akutane na Floyd Mayweather kwa marudiano, pambano ambalo wengi bado
wanalihitaji.
0 comments:
Post a Comment