Mchungaji wa Afrika Kusini Alfred Ndlovu (44) amefariki baada ya kufunga
usiku na mchana kwa siku thelathini akitaka kuvunja rekodi ya Yesu
Kristu aliyefunga siku 40 usiku na mchana bila kula wala kunywa kitu
chochote.
Mchungaji Alfred aliondoka nyumbani kwake tarehe 17/6/2016 na kuelekea nyikani kwa ajili ya kufunga na kuomba, huku akiweka nia kwa Mungu na kujitenga na anasa za ulimwengu. Mchungaji huyu alijulikana kwa imani yake thabiti na familia yake pamoja na jamii iliyomzunguka waliamini imani yake ingeweza hata kuhamisha milima. Kifo chake kimeishangaza jamii nzima likiwemo Kanisa alilokuwa akihudumu.
Akijaribu kuvunja rekodi ya Yesu Kristu, Mchungaji Ndlovu alifariki baada ya kufunga kwa takribani mwezi mzima japokuwa hakuwahi kuripotiwa kuwa na ugonjwa wowote. Alikuwa peke yake nyikani na maiti yake ilionwa na mpita njia aliyetoa taarifa polisi.

0 comments:
Post a Comment