Mchezaji Shiza Kichuya wa Simba
akiwania mpira na mchezaji wa timu ya FC Leopards ya Kenya Kichuya
amefungia Simba goli la tatu dhidi ya timu ya FC Leopards, Magoli mawili
ya mwanzo yamefungwa na mchezaji Ibrahim Ajibu huku Mchezaji Laudit
Mavugo ameongeza goli la nne na kuifanya Simba kutoka uwanjani kifua
mbele kwa magoli 4-0 wakati FC Leopards haijapata kitu katika Tamasha
la Simba Day lililomalizika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
jioni hii.
Simba imefanya tamasha hili ikiwa
na sababu kubwa ya kuwaonyesha na kuwajaribisha wachezaji wao wapya wa
ndani na wa kigeni mara baada ya kuwasajiri kwa ajili ya msimu mpya wa
2016-2017u
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akiwapungia
mikono mashabiki wa simba mara baada ya kukagua vikosi vya timu hizo
kulia ni Evance Aveva Rais wa Simba na kushoto ni Makamu wa Rais wa TFF
Bw. Warrace Kalia
Kikosi cha Timu ya Simba
0 comments:
Post a Comment