Bi. Lorah Madete, Kaimu Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya Uchumi
Jumla, Tume ya Mipango, akitoa neno kwa washiriki wa mafunzo kabla ya
kumkaribisha mgeni rasmi ili afungue mafunzo hayo ya siku tano.
Waliokaa ni Bw. Maduka Paul Kessy, Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya
Uzalishaji, Tume ya Mipango (katikati) na Bw. John Mduma, Mhadhiri
Mwanamizi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mgeni Rasmi Bw. Maduka Paul Kessy, Naibu Katibu Mtendaji, Klasta
ya Uzalishaji, Tume ya Mipango (aliyesimama) akitoa hotuba kwa ajili ya
ufunguzi rasmi wa mafunzo kuhusu Mwongozo wa Usimamizi wa Rasilimali za
Umma kwa washiriki kutoka mikoa ya Mwanza, Mara, Geita and Simiyu.
Wengine ni Bi. Lorah Madete, Kaimu Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya
Uchumi Jumla, Tume ya Mipango (kushoto) na Bw. John Mduma, Mhadhiri
Mwandamizi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (kulia).
Washiriki wa Mafunzo wakimsikiliza kwa makini Mgeni Rasmi
(hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yanayofanyika Jijini
Mwanza katika Ukumbi wa Chuo cha Ufundi Stadi (Veta).
Muwezeshaji Dr. Kenneth Mdadila, Mhadhiri, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akishusha nondo kwa washiriki wa mafunzo hayo.
Washiriki wakisikiliza na kufuatilia kwa makini mafunzo waliyokua wakipata kutoka kwa muwezeshaji.
Washiriki wa
mafunzo kuhusu Mwongozo wa Usimamizi wa Rasilimali za Umma kutoka mikoa
ya Mwanza, Mara, Geita and Simiyu pamoja na wawezeshaji wa mafunzo
wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi mara baada ya ufunguzi wa
mafunzo hayo.
0 comments:
Post a Comment