Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Inj. Mbogo Futakamba na Mtendaji
Mkuu wa Tanzania Water Partnership, Dkt. Victor Kongo wakibadilishana
Hati za Makubaliano ya Utunzaji na Usimamizi wa Rasilimali za Maji
nchini mara baada ya kutia saini.
Wajumbe walioshiriki katika kikao cha kutia saini Hati ya
Makubaliano ya Utunzaji na Usimamizi wa Rasilimali za Maji nchini kati
ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji na Tanzania Water Partnership.
Meneja Mipango, Andrew Takawira (kushoto) na Afisa Mipango,
Michael Raamano kutoka Taasisi ya Global Water Partnership ya Afrika ya
Kusini walikuwa ni miongoni mwa wajumbe wa kikao hicho.
Mtendaji Mkuu wa Tanzania Water Partnership, Dkt. Victor Kongo
akizungumza, kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji, Hamza Sadiki
na Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Inj. Mbogo Futakamba.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Inj.
Mbogo Futakamba akiwa pamoja na Wakurugenzi wa Wizara ya Maji na
Umwagiliaji, wajumbe wa Global Water Partnership na Tanzania Water
Partnership mara baada ya kikao cha kusaini Hati za Makubaliano ya
Utunzaji na Usimamizi wa Rasilimali za Maji nchini.
………………………………………………………….
Wizara ya Maji na Umwagiliaji leo
imesaini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano kati yake na Shirika lisilo
la Serikali, Tanzania Water Partnership (TWP) kwa ajili ya utekelezaji
wa Utunzaji na Usimamizi wa Rasilimali za Maji nchini.
Makubaliano hayo yalisainiwa na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Inj. Mbogo Futakamba na Mtendaji Mkuu wa
Tanzania Water Partnership, Dkt. Victor Kongo na kuhudhuriwa na
wataalamu kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji na wajumbe kutoka
Tanzania Water Partnership.
Lengo kuu la ushirikiano huo
likiwa ni kutunza na kusimamia rasilimali za maji nchini kwa ajili ya
maendeleo endelevu ya upatikanaji wa maji nchini na kuinua kiwango cha
huduma ya majisafi na salama kwa wananchi wote Tanzania.
0 comments:
Post a Comment