TANGOZO

TANGOZO
Latest News
Saturday, September 24, 2016

Faiza Ally: Kila vazi na sehemu yake Tusikariri.

Mrembo na Mjasiriamali Faiza ally, amewataka Watanzania kufahamu na kuelewa kuwa kila vazi linalovaliwa lina sehemu yake.

Akiongea kupitia kipindi cha Hatua Tatu cha Times Fm, wakati akitangaza mchongo wake wa mavazi ya Kuogelea, Faiza amedai watu wasimchukulie vibaya kwa sababu mavazi ya kuogelea anayoyauza yanstahili kwa sehemu husika.

“Kila sehemu na vazi lake nauza zile kwa sababu ni maalum kwa kuogelea tena watoto ndio wateja wangu wakubwa” Alisema.

Mrembo huyo ameweka wazi kuwa baada ya kuiona faida kwenye biashara yake hiyo, amepanga kuongeza wigo na kuanza kuleta Maboya na Miwani maalum za kuogelea pia.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: Faiza Ally: Kila vazi na sehemu yake Tusikariri. Rating: 5 Reviewed By: SIMAMA BUKOBA