TANGOZO

TANGOZO
Latest News
Monday, September 19, 2016

PROFESA MBARAWA AMTEUA DKT. MUSA MGWATU KUWA MTENDAJI MKUU WA WAKALA WA UFUNDI NA UMEME (TEMESA)

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchuzi na Mawasiliano (Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga.
TAARIFA KWA UMMA

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame M. Mbarawa(Mb), amemteua Dkt. Musa Mgwatu kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA).

Dkt. Mgwatu amechukua nafasi ya Mhandisi Marcellin Magesa  ambaye amepangiwa majukumu mengine  Wizarani .

Kabla ya Uteuzi huo Dkt. Mgwatu alikuwa  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika Hodhi la Rasilimali za Reli (RAHCO).

Katika hatua nyingine Profesa Mbarawa amemteua Bw. Masanja Kadogosa ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) Kukaimu nafasi ya Mtendaji Mkuu wa RAHCO.

Uteuzi huo unaanza mara moja.

Imetolewa na
Eng. Joseph M. Nyamhanga
Katibu Mkuu (Ujenzi)

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: PROFESA MBARAWA AMTEUA DKT. MUSA MGWATU KUWA MTENDAJI MKUU WA WAKALA WA UFUNDI NA UMEME (TEMESA) Rating: 5 Reviewed By: SIMAMA BUKOBA