Serikali katika kipindi cha
kuanzia Januari hadi Agosti 2016 imefanikiwa kulipa jumla ya sh. bilioni
511.86 ikiwa ni malimbikizo ya mwajiri kwa watumishi waliostaafu.
Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji alipokuwa akijibu swali la Mary
Chatanda Mbunge wa Korogwe Mjini aliyehoji kuhusu changamoto.
Mary Chatanda Mbunge wa Korogwe mjini inayowakabili wastaafu ya kucheleweshewa mafao yao na Mfuko wa pensheni wa PSPF katika mwaka wa fedha 2015/2016.
“Kucheleweshwa kwa malipo ya
wastaafuhakutokani na Serikali, isipokuwa waajiri ndio baadhi ya nyaraka
zinazohusika ili kuaandaa malipo ya wastaafu hao alisema Dkt. Kijaji.
Naibu Waziri Dkt. Kijaji amesema
kuwa nyaraka zinazomhusu mtumishi ziwasilishwe ndani ya muda wa miezi
mitatu hadi sita kabla ya muda wa kustaafu ili malipo yake yaweze
kuandaliwa kwa wakati na kupata stahili zao ili waweze kukidhi mahitaji
yao ya kila siku.
Aidha, jumla ya sh. bilioni 83.25
zimelipwa ikiwa ni malipo ya deni kabla ya mwaka 1999 hali inayoonesha
kuwa Serikali inaendelea kulipa malimbikizo ya madai ya wastaafu na
mafao mengine yanayotolewa na Mfuko huo ili waweze kuendesha maisha yao
baada ya kustaafu.
Katika kipindi cha mwezi Januari
hadi Julai 2016 Mfuko umelipa mafao ya pensheni ya mwezi kwa kiasi cha
sh. bilioni 117 ambapo kwa sasa mfuko huo unaendelea kulipa malimbikizo
ya mafao ya mkupuo kwa wastaafu wapya na mafao mengine.
Katika kudhihirisha dhamira hiyo
ya kulipa mafao ya wastaafu, Dkt. Kijaji amesema kuwa tangu Julai 2015
bodi za mifuko ya hifadhi za jamii zinaendelea kufanyia kazi mafao ya
wastaafu na kuwalipa stahili zao kwa asilimia 50 kulingana na maelekezo
ya Serikali.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu
Jenista Muhagama ameliarifu Bunge kuwa mfumo na sheria vimeunganishwa na
kutoa fursa kwa mtumishi anapohama kutoka ajira moja kwenda nyingine
anaruhusiwa kuhama kutoka mfuko moja kwenda mfuko mwingine.
0 comments:
Post a Comment