TANGOZO

TANGOZO
Latest News
Wednesday, March 29, 2017

Wafanyabiashara 3 wapandishwa mahakamani Kisutu wakituhumiwa kuingiza nchini makontena ya mitumba yenye magari.

Wafanyabiashara watatu wanaotuhumiwa kuingiza nchni makontena ya mitumba yaliyokuwa na magari wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu na kushindwa kusomewa hati ya makosa baada ya upande wa mashtaka kufanyia mabadiliko ya hati ya mashtaka.

Wafanyabishara hao walifika mahakamani hapo majira ya asubuhi na kukaa mahakamani hapo kwa zaidi ya masaa sita wakiwa chini ya ulinzi na hatimaye kurudishwa polisi ili kupisha muda wa kufanyia mabadiliko hati ya mashtaka.

Akizungumza na vyombo vya habari mmoja wa wakili wa watuhumiwa hao amedai kuwa wateja wake wamelazimika kurudishwa mahabusu kutokana na mabadiliko hayo ya hati ya mashtaka.

Amesema wateja wake wameshikiliwa na polisi kwa muda mrefu na uenda wakafikishwa mahakamani hapo kesho kama upande wa mashtaka utafanikiwa kufanya mabadiliko hayo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: Wafanyabiashara 3 wapandishwa mahakamani Kisutu wakituhumiwa kuingiza nchini makontena ya mitumba yenye magari. Rating: 5 Reviewed By: SIMAMA BUKOBA