Nyota wa muziki Rihanna alibubujikwa
na machozi wakati wa tamasha mjni Dublin usiku wa kuamkia jana baada ya
kuwasili akiwa amechelewa kwa dakika 30 katika ukumbi huo.
Mwanamuziki
huyo alijawa na hisia wakati alipoanza kuimba wimbo wa 'Love The Way
You Lie' aliyoimba kwa ushirikiano na mwanamuziki Eminem.
Mashabiki
waliweka picha na video za mwanbamuziki huuo katika mitandao ya kijamii
wakionyesha wasiwasi wao kuhusu kile kilichotokea.
Rihanna
hakuelezea ni nini kilichotokea mbali na kuandika ujumbe kwatika mtandao
wake wa Instagram akiusifu usiku huo,ilikuwa tamasha iliojaa hisia
kwambgu,aliandika.
''Nina bahati kuwa na kikosi kama vile #Navy man,nimebarikiwa.Ninashukuru sana kwa kuwa nanyi nyote''.#DUBLIN#ANTIWORLDTOUR''
Rihanna
atakuwa nchini Uingereza katika uwanja wa Webly siku ya Ijumaa.Wakati
alipozindua albamu hiyo ,alionekana akiangalia kando na kamera na kuinua
mikono kama ishara ya kutaka kujizatiti.
Lakini mashabiki wake
waliokuwa wamefurika katika tamasha hilo waliendelea kumuimbia hadi
akafuta machozi yake na kuendelea na dakika 80 za kuwatumbuiza.
''Sijawahi kusikia watu wakipiga kelele kwa sauti ya pamoja na hilo limetokea Ireland mjini Dublin'',aliuambia umati.
0 comments:
Post a Comment