TANGOZO

TANGOZO
Latest News
Wednesday, June 29, 2016

SHAMBULIO LA KUJITOA MUHANGA LASABABISHA VIFO UWANJA WA NDEGE UTURUKI

meripotiwa kuwa watu 36 wameuawa katika shambulio la kujitoa muhanga katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Ataturk Istanbul nchini Uturuki na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa, shughuli za usafirishaji katika uwanja huo zimesitishwa huku shughuli ya uokoaji na huduma ya kwanza vikiendelea.
 
Gavana wa mji wa Istanbul amethibisha kuuawa watu haona idadi hiyo ya majeruhi. Mashuhuda wanasema waliwaona washambuliaji watatu ambapo mmoja kati yao alikuwa akifyatua risasi kabla ya kujitoa muhanga kwa kujilipua kwa bomu na kufa.


 Hata hivyo mashambulizi hayo yalihusisha katika eneo la kuingia katika uwanja huo. Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan amelaani shambulio hilo na kusisitiza umoja katika kutokomeza vitendo hivyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: SHAMBULIO LA KUJITOA MUHANGA LASABABISHA VIFO UWANJA WA NDEGE UTURUKI Rating: 5 Reviewed By: SIMAMA BUKOBA