TANGOZO

TANGOZO
Latest News
Tuesday, June 28, 2016

TP MAZEMBE YAIHUKUMU YANGA NYUMBANI 1-0

Bado Yanga wanaendelea kuusaka ushindi wao wa kwanza kwenye hatua ya makundi ya kombe la shirikisho Afrika.

Baada ya kupoteza mechi yao kwanza ugenini dhidi ya MO Bejaia ya Algeria, leo walikuwa nyumbani wakikipiga dhidi ya TP Mazembe mchezo uliomalizika kwa Yanga kupoteza tena kwa goli 1-0.

Goli la Mazembe lilitokana na mpira wa adhabu ndogo baada ya Kelvin Yondani kumuangusha Thomas Ulimwengu nje kidogo ya eneo la hatari. Mpira wa adhabu ndogo ulimfikia Merveille Bope na kuupachika kambani baada ya mabeki wa Yanga kushindwa kuuondosha kwenye eneo lao la hatari.



Yanga-mechi 2 bila goli

Tayari Yanga imeshacheza mechi mbili kwenye hatua ya makundi, wamefungwa zote kwa goli moja (kila mechi) huku wao wakiwa bado hawajafunga bao hata moja katika mechi walizocheza.

Chirwa, Mahadhi, mambo poa

Nyota hawa wa Yanga walikuwa wanacheza mechi yao kwa mara ya kwanza wakiwa Yanga huku Mahadhi akicheza mechi ya kwanza ya kimataifa.

Wote kwa pamoja wameonesha uwezo mkubwa kwa muda waliopata nasi ya kucheza. Mahadhi aliumia na kushindwa kuendelea na mchezo na nafasi yake kuchukuliwa na Geofrey Mwashiuya huku Obrey Chirwa yeye nafasi yake ilichukuliwa na Matheo Athony.



  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: TP MAZEMBE YAIHUKUMU YANGA NYUMBANI 1-0 Rating: 5 Reviewed By: SIMAMA BUKOBA