TANGOZO

TANGOZO
Latest News
Sunday, June 26, 2016

TIMU YA VIJANA CHINI YA MIAKA (17) SERENGETI BOYS IMEPATA USHINDI WA MAGOLI 3-0


Timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ imepata ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Seychelles katika mchezo wa kuwania kushiriki fainali za mataifa ya Afrika kwa vijana.
Nickson Kabage, Ibrahim Abdallah na Ally Hussein ndiyo walifunga magoli ya Serengeti Boys kwenye mchezo huo.
Ushindi huo umemgusa pia Waziri mwenye dhamana ya michezo Mh. Nape Nnauye ambaye hakusita kuwapongeza vijana kwa ushindi walioupata.

“Kwanza tukubali kwamba wamecheza vizuri sana, wamecheza zaidi ya kile ambacho nilikuwa nakitarajia. Tunaamini mwanzo wao ni mzuri, walikwenda kwenye mashindano India na kufanya vizuri, wamefanya vizuri hapa na tunatarajia watafanya vizuri watakapokwenda Seychelles,” amesema Nnauye wakati akitoa pongezi zake kwa Serengeti Boys.
“Tunayo matumaini makubwa na vijana hawa, kwanza nitoe wito kwamba ni vizuri tukaona matumaini yanayooneshwa na vijana hawa na tujitokeze kuwekeza kwao . Uwekezaji huu umeanza vizuri niwapongeze wote waliotufikisha hapa lakini pia nitoe wito kwa wengine sasa wawekeze ili twende mbali zaidi.”
“Sijawaahidi chochote lakini tunayo ya kufanya na tutafanya kupitia TFF.”

Serengeti Boys inatarajiwa kuondoka June 30 kuelekea Seychelles ambako kwa ajili ya mchezo wa marudiano July mbili .
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: TIMU YA VIJANA CHINI YA MIAKA (17) SERENGETI BOYS IMEPATA USHINDI WA MAGOLI 3-0 Rating: 5 Reviewed By: SIMAMA BUKOBA