TANGOZO

TANGOZO
Latest News
Friday, July 22, 2016

CAF YAPATA MDHAMINI MPYA

Shirikisho la Soka barani Africa (CAF) limepata mdhamini mpya baada ya kumalizika kwa mkataba wake na kampuni ya mawasiliano ya Orange.




Kabla ya hapo, kampuni nyingine ya mawasiliano ya MTN ndiyo iliyokuwa mdhamini kwa miaka minne.


Sasa, mdhamini mpya atakuwa kampuni ya mafuta na gesi ya Total kutoka Ufaransa.

Kampuni hiyo itaanza kwa kudhamini michuano ya Kombe la Taifa Bingwa Afrika mwaka 2017 ambayo itaandaliwa nchini Gabon.

Thamani ya mkataba huo haijafichuliwa.

Total itakuwa mdhamini mkuu wa:

  • Kombe la Taifa Bingwa Afrika
  • Ligi ya Klabu Bingwa Afrika
  • Kombe la Taifa Bingwa Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN)
  • Super Cup ya Afrika
  • Kombe la Mashirikisho
  • Kombe la Taifa Bingwa Afrika kwa Wanawake
  • Kombe la Futsal Afrika
  • Kombe la Taifa Bingwa Afrika wachezaji wa chini ya miaka 23
  • Kombe la Taifa Bingwa Afrika wachezaji wa chini ya miaka 20
  • Kombe la Taifa Bingwa Afrika wachezaji wa chini ya miaka 17
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: CAF YAPATA MDHAMINI MPYA Rating: 5 Reviewed By: SIMAMA BUKOBA