TANGOZO

TANGOZO
Latest News
Thursday, July 21, 2016

GOMEZI HATAKI KUKAA TENA UTURUKI

Mshambuliaji wa Ujerumani Mario Gomez amesema hatakaa tena nchini Uturuki kutokana na machafuko ya kiasiasa yaliyotokana na jaribio la mapinduzi ya serikali wiki iliyopita.

Gomez amekuwa akichezea klabu ya Besiktas ya Istanbul ambapo aliwafungia mabao 28 katika mechi 41.

Klabu hiyo ilishinda taji la ligi ya Uturuki msimu uliomalizika majuzi.

Alikuwa kwenye klabu hiyo kwa mkopo kutoka Fiorentina ya Italia.

"Hakuna sababu za kimichezo au sababu nyingine za kando ambazo zimenifanya kuchukua uamuzi huu,” Gomez, 31, amesema kwenye Facebook.

Gomez alikuwa ameafikiana kukaa kwa mkopo Besiktas kwa mwaka mmoja, na kulikuwa na uwezekano wake kuhamia kikamilifu kwenye klabu hiyo baada ya kipindi hicho cha mkopo.

Gomez alichezea Ujerumani katika Euro 2016 na akawafungi mabao mawili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: GOMEZI HATAKI KUKAA TENA UTURUKI Rating: 5 Reviewed By: SIMAMA BUKOBA