TANGOZO

TANGOZO
Latest News
Thursday, July 21, 2016

KIONGOZI WAUPINZANI AFUNGWA JERA GAMBIA

Kiongozi wa upinzani nchini Gambia Ousainou Darboe ameuhukumiwa kufungwa jela miaka mitatu.

Bw Darboe amehukumiwa pamoja na watu wengine 18 baada ya kupatikana na makosa kadha yanayohusiana na maandamano yaliyofanywa dhidi ya serikali mwezi Aprili.

Maandamano hayo yaliongozwa na Bw Darboe.

Kiongozi huyo wa upinzani alikuwa akishiriki maandamano hayo kulalamikia taarifa za kuuawa kwa mmoja wa viongozi wa chama chake, Solo Sandeng, akiwa kizuizini.

Maandamano huwa nadra sana nchini Gambia, ambayo imetawaliwa na Rais Yahya Jammeh tangu achukue madaraka kupitia mapinduzi ya kijeshi 1994.

Uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika Desemba, lakini viongozi wa upinzani wanasema hautakuwa huru na wa haki.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: KIONGOZI WAUPINZANI AFUNGWA JERA GAMBIA Rating: 5 Reviewed By: SIMAMA BUKOBA