TANGOZO

TANGOZO
Latest News
Thursday, July 21, 2016

MTU MWEUSI AFARIKI MIKONONI MWA POLISI UFARANSA

Maafisa wa polisi katika mji wa Beaumont-sur-Oise, Ufaransa wamekabiliana na waandamanaji baada ya kijana mweusi kufariki akiwa kizuizini.

Mabomu ya petroli yamerushiwa maafisa wa polisi na taarifa zinazema waandamanaji walijaribu kuteketeza ukumbi wa mji.

Watu wanane wamekamatwa na kuzuiliwa.

Polisi wanasema Adama Traore alipata mshtuko wa moyo Jumanne baada yake kuzuiliwa katika mji huo ulioko kilomita thelathini kaskazini mwa Paris.

Lakini marafiki zake wanasema alikuwa buheri wa afya kabla ya kukamatwa na kwamba alipigwa na maafisa hao wa polisi.

Uchunguzi wa kubaini chanzo cha kifo chake utafanywa baadaye Alhamisi.

Miaka 11 iliyopita, vifo vya vijana wawili waliokuwa wakijaribu kukwepa kukamatwa vilisababisha maandamano yaliyodumu wiki mbili katika viunga vya mji wa Paris na miji mingine nchini humo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: MTU MWEUSI AFARIKI MIKONONI MWA POLISI UFARANSA Rating: 5 Reviewed By: SIMAMA BUKOBA