TANGOZO

TANGOZO
Latest News
Saturday, July 30, 2016

KOFFI OLOMIDE ANYIMWA DHAMANA

Mwanamuziki maarufu Koffi Olomide amekatazwa dhamana ya kuachiliwa huru kulingana na wakili wake.

Jaji alikataa ombi lake la la kuachiliwa wakati alipowasilishwa mahakamani.

Siku ya Jumatatu ,maafisa wa polisi walimkamata Olomide mwenye umri wa miaka 60 nyumbani kwake katika makaazi ya Kinshasa baada ya kupatikana katika kamera akimpiga teke mmoja wa wanenguaji wake katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta mjini nairobi.

Alirejeshwa nchini DRC kutoka Kenya kufuatia kisa hicho cha Ijumaa.

Hatua hiyo ilisababisha kufutiliwa mbali kwa tamasha lake nchini Kenya na Zambia.
Amekana mashtaka yanayomkabili

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: KOFFI OLOMIDE ANYIMWA DHAMANA Rating: 5 Reviewed By: SIMAMA BUKOBA