Mkufunzi mpya wa Manchester City,Pep Guardiola, amesajili ushindi wake wa kwanza tangu atue Manchester City baada ya kuwaongoza mabingwa hao wa zamani wa ligi kuu ya Uingereza kuwalaza Borussia Dortmund katika kinyang'anyiro cha kutafuta mabingwa wa vilabu vya kimataifa huko China.
Kipa chipukizi wa Man City
Angus Gunn, 20, aliokoa mkwaju wa penalti wa Mikel Morino na
kuwahakikishia vijana wa Pep ushindi wa mabao 6-5.
Mechi hiyo iliyochezwa katika uwanja wa Longgang ulioko Shenzhen ilikuwa imeishia sare ya 1-1 katika muda wa kawaida.
Sergio Aguero alikuwa ameiweka Man City kifua mbele mapema katika
mechi hiyo lakini mshambulizi chipukizi wa Dortmund Christian
Pulisic, mwenye umri wa miaka 17, kuwasawazishia wajerumani hao katika
muda wa majeruhi.
Hii ndio ilikuwa mechi ya kwanza kwa Man City
baada ya mechi iliyokuwa imepangwa awali dhidi ya vibonde wao wa jadi
kutoka Uingereza Manchester United kuahirishwa kufuatia mvua kubwa
iliyonyesha mjini Beijing.
0 comments:
Post a Comment