TANGOZO

TANGOZO
Latest News
Thursday, July 28, 2016

PETER OKOYE WA PSQUARE AOMBA RADTI MASHABIKI

Mwanamuziki wa Nigeria anayeunda kundi la Psquare Peter Okoye ameomba msamaha kwa washabiki kufuatia ugomvi na kaka yake.

Kupitia video iliyosambaa katika mitandao ya kijamii amesema timu nzima ya Psquare kwa sasa imerudi tena pamoja.

Akiwa amevalia kofia ndani ya gari, video hiyo inamuonesha Okoye ni mwenye kujuta, akisema kuwa anabeba jukumu kwa yote yaliyotokea.

Peter alikuwa na uhasama na pacha wake Paul, ambaye ndiye amekuwa akiimba naye kwa zaidi ya muongo mmoja, hali iliyofanya kugawa kundi hilo.

Kulikuwa na dalili kwamba utengano wao huo unahatarisha mafanikio ya mapacha hao.

Peter na Paul ambao wanapiga muziki wa hiphop wametoa nyimbo nyingi zilizovuma ndani ya Nigeria na nchi nyingine za Afrika.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: PETER OKOYE WA PSQUARE AOMBA RADTI MASHABIKI Rating: 5 Reviewed By: SIMAMA BUKOBA