Msanii Snura Mushi aliyewahi kuwika na nyimbo
mbalimbali, ameibuka na kudai kwamba ana mpango wa kutoa filamu moja
mwakani.
Snura alisema baada ya kuingia katika muziki amekuwa na shoo nyingi
kiasi kwamba hukosa muda wa kuigiza, licha ya mashabiki wake kumtaka
afanye hivyo hata kwa mara moja.
“Mashabiki wangu wamekuwa wakinitaka angalau nicheze hata filamu
nmoja, lakini shoo za muziki zimekuwa nyingi nakosa muda wa kuigiza,
lakini nitapanga mwakani nitoe filamu moja kwa ajili ya mashabiki wangu
huku nikiendelea na muziki,’’ alisema Snura, ambaye amekuwa akiingiza
fedha nyingi kupitia shoo zake za mara kwa mara mikoa mbalimbali.
Snura ameigiza filamu mbalimbali na mwanzo wa safari yake ya sanaa aliwahi kuwa kundi moja na marehemu Sharo Milionea na Kitale.
0 comments:
Post a Comment