TANGOZO

TANGOZO
Latest News
Monday, July 25, 2016

RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI MWINGINE LEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Samuel M. Nyantahe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC).

Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Uteuzi huu umeanza July 20 2016. 

 Kabla ya uteuzi huo Dkt. Samuel M. Nyantahe alikuwa Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI). Dkt. Samuel M. Nyantahe anachukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Chrisant Majiyatanga Mzindakaya ambaye amejiuzulu wadhifa huo.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI MWINGINE LEO Rating: 5 Reviewed By: SIMAMA BUKOBA