Mtaalam na Mkufunzi wa masuala ya
Afya kutoka Makao Makuu ya Shirika la Afya Duniani (WHO)
Geneva,Switzarland Olau Poppe akitoa mafunzo kwa Timu ya wataalam wa
Afya kutoka nchi zipatazo 14 za Bara la Afrika kuhusu mfumo wa taarifa
unaotumika kutambua sababu za kifo cha mgonjwa kuwajengea uwezo watalaam
hao uelewa wa ujazaji wa taarifa sahihi juu ya sababu ya kifo cha
mgonjwa kwenye cheti cha kifo (Death Certificate) ili wakatoe mafunzo
kwa wataalam wengine kwenye nchi zao. Mafunzo hayo ya Siku mbili
yanafanyika jijini Dar es salaam.
Mtaalam na Mkufunzi wa masuala ya
Afya kutoka Makao Makuu ya Shirika la Afya Duniani (WHO) Geneva, Olau
Poppe akifuatilia majadiliano ya washiriki wa mafunzo ya siku 2 ya
wataalam wa Afya kutoka nchi zipatazo 14 za Bara la Afrika kuhusu mfumo
unaotumika kutambua sababu ya kifo cha mgonjwa utakaowasaidia watalaam
hao kujaza taarifa sahihi kwenye cheti cha kifo.
Baadhi ya Washiriki wa mafunzo kwa
Timu ya wataalam wa Afya kutoka Tanzania, Zambia na Cameroon
wakifuatilia miongozo mbalimbali iliyokuwa inatolewa na watalaam kutoka
Makao Makuu ya Shirika la Afya Duniani (WHO) wakati wa Mafunzo kuhusu
mfumo wa taarifa unaotumika kutambua sababu za kifo cha mgonjwa
kuwawezesha watalaam hao kujaza taarifa sahihi juu ya sababu ya kifo cha
mgonjwa leo jijini Dar es salaam.
0 comments:
Post a Comment