TANGOZO

TANGOZO
Latest News
Wednesday, July 20, 2016

TANZANIA YA FAFANUA KUHUSI MLIMA KILIMANJARO

Bodi ya Utalii Tanzania imetoa taarifa kufafanua kuhusu Mlima Kilimanjaro baada ya shirika moja la habari la Marekani kudaiwa kuchapisha taarifa iliyoonekana kuashiria mlima huo unapatikana Kenya.

Shirika hilo lilikuwa likiripoti kuhusu kifo cha Guguleth Zulu, raia wa Afrika Kusini, aliyefariki akikwea Mlima Kilimanjaro.
“Tungependa kusahihisha habari za kupotosha zilizochapishwa na Miami Herald, kwamba Mlima Kilimanjaro unapatikana Tanzania na si Kenya,” taarifa iliyotiwa saini na meneja mkurugenzi wa Bodi ya Utalii ilisema.

Bodi hiyo inasema imeliandikia barua gazeti hilo na kulitaka lichapishe sahihisho.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: TANZANIA YA FAFANUA KUHUSI MLIMA KILIMANJARO Rating: 5 Reviewed By: SIMAMA BUKOBA