Ripoti mpya kuhusu utumikishaji
watoto nchini Tanzania iliyozinduliwa hii leo inaonyesha asilimia 28 ya
watoto wote wa nchi hiyo wanatumikishwa katika kazi ngumu na za hatari.
Kwa
mujibu wa ripoti hiyo watoto hao wamekuwa wakitumikishwa katika maeneo
hatarishi kama vile kwenye migodi ya madini, kilimo, misitu na uvuvi.
Hata
hivyo ripoti hiyo inaonyesha kupungua kidogo kwa tatizo hilo
ikilinganishwa na miaka kumi iliyopita ambapo watoto waliokuwa
wakitumikishwa nchini humo walikuwa ni asilimia 30 ya watoto wote.
Takwimu
zilizotolewa leo na ofisi ya taifa ya takwimu kwa kiasi fulani
zinaonyesha matumaini kwa watoto ambao ni taifa la kesho huku lengo
kubwa kwa nchi hiyo likiwa ni kutimiza azma ya malengo endelevu ya
maendeleo ya dunia ya kuondoa kabisa tatizo hili ifikapo mwaka 2030.
Mkurugenzi mkuu ofisi ya taifa ya Takwimu nchini Tanzania Dkt Albina
Chuwa,amesema kama ilivyo kwa tafiti zilizopita, lengo kubwa ni kupata
viashiria mbalimbali vinavyoonyesha hali halisi ya utumikishwaji watoto
nchini humo.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyotolewa hii leo
utumikishwaji wa watoto nchini Tanzania umepungua kwa asilimia 2.8
ikionyesha mafanikio tokea takwimu za mwaka 2006.
Mojawapo ya njia zinazotumiwa na serikali ya Tanzania kuondoa utumikishwaji wa watoto ni ni uanzishwaji wa elimu bure.
0 comments:
Post a Comment