Mwanamume mmoja wa Nigeria
aliyekamatwa kwa kumuita mbwa wake jina la rais Muhamadu Buhari
amewachiliwa huru bila ya kushtakiwa,kulingana na chombo cha habari cha
Vanguard.
Joe Fortemose Chinakwe aliambia mtandao huo kwamba hakuwa na lengo la kumtusi rais alipomtaja mbwa wake jina la rais huyo.
Amesema kwake anaona kwamba ni sifa kubwa kwa kuwa anapendelea maamuzi ya rais huyo.
''Nilimuita
mbwa wangu jina la rais kwa kuwa yeye ni shujaa wangu.Nilianza kumpenda
Buhari wakati alipokuwa rais mwanajeshi hadi leo ambapo amekuwa
raia.Baada ya kusoma kuhusu maamuzi yake dhidi ya ufisadi unaokula
uchumi wa taifa hili ,niliamua kulibadilisha jina la mbwa wangu ambye
nilimuita Buhari.Sikujua kwamba nilikuwa nafanya makosa kwa kumpenda
Buhari''.
0 comments:
Post a Comment