Bi harusi, ambaye kakake alifariki
wiki chache kabla yake kufunga ndoa, amechukua hatua isiyo ya kawaida
kwa kuongeza picha za kakake huyo katika zake za harusi Uingereza.
Kakake
Catherine Carter, Shaun Carter, alifariki kwenye ajali Mei lakini
alipofunga pingu za maisha Julai aliomba usaidizi kutoka kwa mtaalamu wa
picha kuongeza picha za Shaun kwenye picha za harusi.
Katika
picha moja, Catherine anaonekana akiwa na mamake na babake wa kambo na
kunayo picha ambayo haijakolea sana na nduguye anayeoneakana kuweka
mikono yake kwenye bega la Catherine.
Alisema: "Ni mwujiza kumuona kwenye picha zangu za harusi, sikuweza kujizuia kutokwa na machozi."
Seeing him in the pictures was a miracle, I couldn't stop crying."
Shaun, 29, alifariki katika ajali eneo la mjengo Cirencester, eneo la Gloucestershire, mwishoni mwa mwezi Mei.
Catherine, aliolewa na John Flower katika kanisa la St Paul's, Chippenham mwezi Julai.
Rachel, wa kampuni ya Jelly Penguin Graphics, ambayo iliunda picha hizo, amesema ombi la Catherine lilimgusa sana.
Tangu picha hizo zipakiwe kwenye Facebook, zimependwa na zaidi ya watu 2,000 na mamia ya watu wametolea maoni.
0 comments:
Post a Comment