TANGOZO

TANGOZO
Latest News
Wednesday, August 10, 2016

BUZWAGI YAKABIDHI SHULE MPYA NA NYUMBA ZA WALIMU KWA SERIKALI WALAYANI KAHAMA

 Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo akifafanua jambo kwa wajumbe wa kamatiya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kahama wakati wa ziara ya kupokea miradi ya maendeleo.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu (aliyeweka mkono kwenye mfuko wa suruali) akiwa na wajumbe wengine wa kamati ya ulinzi na Usalama wa wilaya ya Kahama walipofanya ziara katika mgodi wa Buzwagi wa kukabidhiwa miradi ya maendeleo. 

Meneja Mkuu wa Mgodo wa Buzwagi Asa Mwaipopo akieleza jambo kwa wajumbe wa kamati ya ulinzi na Usalama wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu.

Kifaa maalumu cha kupoza umeme ambacho kitatumika kupeleka umeme katika mji wa Kahama na kungunguza tatizo la kukosekana kwa umeme kikiwa kimefungwa katika kituo cha Umeme cha mgodi wa Buzwagi.

Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo (Mwenye kofia ya blue) akitoa maelezo kwa mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu (mwenye kofia ya kaki) wakati wa makabidhiano ya madarasa ya shule mpya ya msingi ya Budushi, wengine katika picha ni mbunge wa kahama mjini Mhe.Jumanne Kishimba na Mwenyekiti wa halmashauri ya mji Kahama Mhe.Abel Shija. 

Mkuu wa wilaya Kahama Fadhili Nkurlu na Mbunge wa Kahama Mhe.Jumanne Kishimba wakizindua majengo ya shule mpya ya Budushi iliyojengwa kwa ufadhili wa mgodi wa Buzwagi.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu na Mwenyekiti wa kijiji cha Budushi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa majengo na nyumba moja ya walimu katika shule hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Kahama, Fadhili Nkurlu (mwenye kofia ya kaki) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Mgodi wa Buzwagi na Watendaji wa Kata ya Mwendakulima.
 Moja ya majengo ya madarasa yaliyojengwa katika Shule ya Msingi Budushi chini ya ufadhili wa Mgodi wa Buzwagi.
Mkuu wa wilaya ya Kahama, Fadhili Nkurlu akiteta jambo na baadhi ya viongozi wa kata ya Mwendakulima.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: BUZWAGI YAKABIDHI SHULE MPYA NA NYUMBA ZA WALIMU KWA SERIKALI WALAYANI KAHAMA Rating: 5 Reviewed By: SIMAMA BUKOBA