TANGOZO

TANGOZO
Latest News
Monday, August 29, 2016

Fabregas akana kukosana na mkufunzi Conte


Kiungo wa kati wa Chelsea Cesc Fabregas amepinga madai kwamba alikosana na meneja wa klabu hiyo Antonio Conte.

Meneja huyo aliripotiwa kumtaka mchezaji huyo wa miaka 29 kuondoka kabla ya kukamilika kwa siku ya mwisho ya uhamisho.

Fabregas hatahivyo amechapisha katika mitandao ya kijamii akisema kuwa wawili hao wana uhusiano mzuri na kwamba ataendelea kuichezea Chelsea.

'Mbali na ilivyoandikwa, mkufunzi Conte hajawahi kuniambia kwamba niondoke '',aliandika Fabregas.

''Aliniambia kwamba ananitegemea na mimi namtegemea.Nitaendelea kuichezea klabu hii hadi mwisho na iwapo nitahitajika nitajitolea''.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: Fabregas akana kukosana na mkufunzi Conte Rating: 5 Reviewed By: SIMAMA BUKOBA