Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupa pingamizi la Mkurugenzi
wa Kampuni ya Tiptop Connections ya jijini Dar es Salaam, Hamis Shaban
Taletale, maarufu Babu Tale, na kumtaka ajieleze ni kwa nini asifungwe
jela baada ya kushindwa kulipa fidia ya Sh250 milioni.
Uamuzi huo umetolewa na Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es
Salaam, Projest Kahyoza baada ya kutupilia mbali pingamizi la Babu Tale,
ambaye pia ni Meneja wa Msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya
nchini, Abdul Nassib maarufu kama Diamond Platnum.
Babu Tale aliweka pingamizi kupitia jopo la mawakili wake wanne,
akipinga amri ya kukamatwa na kufikishwa mahakamani akidai taratibu za
kisheria za kumkamata na kumfikisha mahakamani hazikufuatwa.
Alikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa amri ya mahakama, baada ya
kushindwa kufika kusikiliza maombi ya utekelezaji wa hukumu ya mahakama
hiyo iliyomwamuru yeye na ndugu yake, Idd Shaban Taletale kulipa fidia
ya Sh250 milioni katika kesi ya ukiukaji hakimiliki.
Kesi hiyo ilifunguliwa na Mhadhiri wa Dini ya Kiislamu, Sheikh
Hashimu Mbonde dhidi ya kampuni ya Tip Top Connections inayomilikiwa na
ndugu hao baada ya kutumia mahubiri yake kibiashara bila ridhaa yake.
Mahakama imetupilia mbali pingamizi hilo baada ya mmoja wa mawakili
wake, Mugaya kutokufika mahakamani huku wengine waliokuwapo wakiomba
usikilizwaji uahirishwe hadi tarehe nyingine. Baada ya kutupilia mbali
pingamizi hilo, Msajili Kahyoza aliamuru Babu Tale afike mahakamani
Agosti 24 ili ajieleze ni kwa nini asifungwe jela kutokana na kushindwa
kutekeleza hukumu hiyo ya Mahakama.
Kwa upande wa Babu Tale, Jumatano hii alipost ujumbe ambao ulionyesha ni jinsi gani yupo kwenye kipindi kigumu.
“There’s no permanent situation in life. Yataisha kama yalivyo anza!,” aliandika Babu Tale kupitia istagram yake.
0 comments:
Post a Comment