Hatimaye ahadi ya shabiki wa Simba, ambaye ni Mkurugenzi wa
Makampuni ya Mohammed Enterprises (MeTL Group), Mohammed Dewji
amekamilisha ahadi aliyoisema kabla ya mkutano mkuu wa Simba kwa
kukabidhi Milioni 100 kwa uongozi wa Simba kwa ajili ya kufanya usajili.
MO amekabidhi pesa hizo baada ya kueleza mipango yake kwa
Simba ya kuwa kama wanachama wa Simba wataridhia kufanya mabadiliko basi
atachangia pesa ya usajili jambo ambalo katika mkutano wake wa Jumatatu
na waandishi wa habari kuwa ahadi yake ni kweli na ataikamilisha kabla
ya dirisha la usajili kufungwa.
Akizungumza baada ya kupokea cheki kutoka kwa MO, Rais wa
Simba, Evans Aveva, amemshukuru MO kwa msaada huo na sasa wanasimba
watatembea kwa kujiamini kwani wamepata pesa ya kufanya usajili.
“Nakushukuru MO kwa msaada ambao umetupatia tunaamini ni
mapenzi ambayo unayo kwa Simba ndiyo umefanya uwe tayari kutoa pesa hizi
na sisi tunaamini zitaweza kutusaidia kupiga hatua na hata tuweze
kutembea kifua mbele,” alisema Aveva.
Aidha Aveva alisema kiasi hicho cha pesa bado hakijatosha kwa
kufanya usajili ambao wamepanga kuufanya lakini kitawasaidia kupiga
hatua ya kufanya usajili ambapo kwa msimu huu wamepanga bajeti ya
Milioni 400 lakini pia kumtaja mchezaji wa Ivory Coast ambaye wanataka
kumsajili ni Fredrick Blagnon.
Kwa uapnde wa MO alisema ametoa msaada huo kama sehemu ya
ahadi aliyoitoa kabla ya mkutano mkuu na hakuna makubaliano yoyote
lakini pia kuwapa ahadi mashabiki wa Simba kuwa kama akipata nafasi
ataweka bajeti zaidi ya Bilioni 1 kwa mwaka kwa ajili ya usajili
0 comments:
Post a Comment