Mahakama ya kikatiba ya Indonesia inajadili iwapo mapenzi ya jinsia moja yanafaa kuwa uhalifu.
Mahakama hiyo ya juu ilikubali ombi lililowasilishwa na kundi moja la wanaharakati wa Kiislamu Family Love Alliance.
Mapenzi
ya jinsia moja ni halali katika maeneo mengi ya Indonesia ,lakini
wapenzi wa jinsia moja wamekuwa wakibaguliwa katika kipindi cha mwaka
mmoja baada ya viongozi kadhaa wa kidini kuikana jamii hiyo.
Mtandao
wa mahakama hiyo unasema kuwa utasikiliza ushahidi kutoka kwa maafisa
wa afya ambao wanaamini kwamba mapenzi ya jinsia moja yanaweza kueneza
magonjwa ya zinaa,lakini wakosoaji wanasema kuwa hayo hutokea hata
miongoni mwa wasioshiriki katika mapenzi hayo.
0 comments:
Post a Comment