TANGOZO

TANGOZO
Latest News
Tuesday, August 2, 2016

UPASUAJI WA (APPENDIX) UNAONGEZA UZAZI: UTAFITI

Utafiti umebaini kuwa wanawake ambao wametolewa kidole tumbo ama 'appendix' au kutolewa kifindofindo au kifuko ama ''Tonsils'' kwa njia ya upasuaji wanapata uwezo mkubwa zaidi wa kushika mimba.

Utafiti huo wa miaka kumi na tano, uliyofanywa katika chuo kikuu cha Dundee,ulihusisha uchunguzi wa rekodi za matibabu ya zaidi ya wanawake nusu milioni wa Uingereza.

Utafitu huu unawapa akina mama wanatafuta ujauzito afueni kubwa sana na pia kuwaondolewa wasiwasi kuhusu uoga wa kufanyiwa opereshini ya kuondolewa kidole tumbo yani appendix kwamba eti itahitalafiana na uwezo wao wa kupata uja uzito.

Utafiti huu huo pia ilifanyiwa wanawake nusu milioni waliofanyiwa operesheni ya kuondolewa kifindo findo au tonsils kwa kiingereza kama kweli inaleta utasa miongoni mwa wanawake.

Mmoja ya watafiti hao Daktari Sami Shimi anasema madakatari wengi walipotoshwa walipokuwa chuoni wakisomea udakatari.

''Chuoni tulielezwa kuwa kufanyiwa oparesheni ya kuondolewa kidole utumbo yaani apendix inasababisha utasa na kumfanya mwanamke asiweze kupata ujauzito''.
 Mtafiti huyo ameiambia BBC kuwa oparesheni ya kuondoa kifindo findo au hata kuondoa kidole tumbo ,apendix haisababishi utasa.

Na wamethibitisha hali hii baada ya kuwafanyia utafiti jumla ya wanawake nusu milioni nchini Uingereza.

Daktari Sami anasema utafiti huu unawahakikikisha wasichana kwamba wakiwa na matatizo ya 'appendix' au kidole tumbo wasiwe na wasiwasi kwamba itapunguza uwez\o wao wa kupata uja uzito siku za baadae.

Badala yake mwanasayansi huyo wa maumbile anasema badala yake kufanyiwa upasuaji wa kuondoa 
sehemu hizo za mwili zikiwa zinauma au kutatiza au hata zikiwa zinapata maambukizi ya mara kwa mara inamuongezea mwanamke uwezo wa kujaliwa kupata mimba.

ena kwa haraka sana.

Wanasayansi hawa wanaujumbe maalum tena wa matumaini kwa akina mama.

Nao wanasema hivi , Pengine tatizo lako la kutoweza kuzaa wewe mama linasababishwa na matatizo ya kidole tumbo yaani appendix au huenda unamatatizo ya muda mrefu ya kifindofindo , tonsils, basi harakisha uende ukafanyiwe upasuaji wa kuondoa Apendix na Tonsils ili uongeze uwezo wako wa kupata ujauzito na kujaaliwa na watoto.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: UPASUAJI WA (APPENDIX) UNAONGEZA UZAZI: UTAFITI Rating: 5 Reviewed By: SIMAMA BUKOBA