Upinzani nchini Zambia umeshutumu
mamlaka ya uchaguzi kwa mipango ya kumpendelea Rais Edgar Lungu na
kusema watapinga matokeo hayo katika Mahakama ya Katiba.
Rais wa chama cha Movement for Multiparty Democracy, Dk Nevers Mumba, amesema analo mkononi pingamizi la kuzuia matokeo yasitangazwe, jambo ambalo lilipuuzwa na tume.
“tulienda mahakamani Jumapili na tukapewa pingamizi la kuzuia tume ya uchaguzi isiendelee kutangaza matokeo ya uchaguzi na wakapuuza agizo la mahakama na kuendelea kutangaza kura zenye mgogoro ambazo zinatonyesha kuwa wanaongoza dhidi yetu, kwasababu tumekuwa tukiongoza muda wote, kama kusingekuwa na wizi wa kura”.
Amesema chama chake kimewakamata watu tofauti wakichezea karatasi za kupigia kura na kwa sababu hiyo hivi sasa wapo chini ya ulinzi.
0 comments:
Post a Comment