TANGOZO

TANGOZO
Latest News
Thursday, August 4, 2016

VYUO 175 NCHINI VYAPEWA NOTISI YA KUSHUSHWA HADHI

Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), Mhandisi Steven Mlote(kushoto)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,wakati wa alipokuwa akitoa tamko la baraza hilo juu ya kuvifutia Usajili baadhi ya vyuo ambapo kati ya 175 vimepewa notisi ya kushushwa hadhi na 5 vimefutiwa Usajili na 41 vimetakiwa kujisajili mara moja ,ikiwa katika jitihada za kuboresha elimu ya ufundi nchini,Katikati Kaimu wa baraza hilo Dkt. Adolf Rutayuga na Mkurugenzi wa Udhibiti,Ufuatiliaji na Tathimini Bi. Agness Ponera.
 

Baadhi ya wafanyakazi wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) wakiwa kwenye mkutano wakati Mwenyekiti wa Baraza hilo Mhandis Steven Mlote(hayupo pichani)alipokuwa akiongea na waandishi habari jijini Dar es Salaam kuhusiana na tamko la baraza hilo kuvifutia Usajili baadhi ya vyuo ambapo kati hivyo 175 vimepewa notisi ya kushushwa hadhi na 5 vimefutiwa Usajili na 41 vimetakiwa kujisajili mara moja,ikiwa katika jitihada za kuboresha elimu ya ufundi nchini.
 
………………………………………………………………………………………………………
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) limetangaza kuwa vyuo 5 vimefungwa kuendesha mafunzo na kufutwa kwenye rejista ya vyuo vya ufundi nchini.

Pia Baraza limetangaza kuwa vyuo 41 vinavyotoa elimu ya ufundi bila kusajiliwa kwa mujibu wa sheria vimepewa muda wa wiki mbili na kutakiwa vijisajili mara moja kwenye Baraza hilo kabla ya kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Vilevile, vibali vya  usajili wa vyuo 112 vya kutoa elimu ya ufundi vimefikia ukomo hivyo vinapaswa kutekeleza masharti ya Usajili; wakati  vyuo 57 vimefikia ukomo wa ithibati, hivyo inapaswa kutekeleza masharti ya ithibati, imetangazwa jana.

Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Baraza (NACTE), Mhandisi Steven Mlote, amesema Baraza limetoa muda wa mwezi mmoja kwa vyuo 112 kutekeleza masharti ya usajili na vyuo 52 kutekeleza masharti ya ithibati kwa mujibu wa sheria za uendeshaji vyuo vya ufundi nchini, na vyuo vitakavyoshindwa kutekeleza agizo hili vitafungiwa mara moja.

Mhandisi Mlote pia alitoa onyo akisema “vyuo 41 vinavyotoa elimu ya ufundi bila kusajiliwa kwa mujibu wa sheria nimevipa muda wa wiki mbili na navitaka vijisajili mara moja kwenye Baraza kabla ya kuchukuliwa hatua kali za kisheria”.

Mhandisi Mlote alivitaja vyuo vyote vyenye matatizo kama ifuatavyo:
Jedwali I: Vyuo vya Ufundi Vilivyofutiwa Usajili
NA. CHUO
  State College of Health and Allied Sciences – Dar es Salaam
  Zoom Polytechnic College – Dar es Salaam
  Tabitha College – Dar es Salaam (formerly: Thabita Vocational Training College – Dar es Salaam)
  Financial Training Centre – Dar es Salaam
  TMBI College of Business and Finance – Dar es Salaam
Jedwali II: Vyuo ambavyo Havijasajiliwa na vinavyoendesha Programu zisizo na Kibali cha Baraza

NA. CHUO
1.        King Solomoni College – Arusha
2.        Avocet College of  Hotel Management – Arusha
3.        Kewovac Nursing Training Centre – Mbagala, Dar es Salaam
4.        St. Family Health Training Institute – Mbagala, Dar es Salaam
5.        Bethesda Montessori Teachers Training College – Arusha
6.        Green Themi Teacher’s College & Green Themi Institute of Tourism
7.        Mainland Institute of Professionals – Arusha
8.        St. David College of Health – Dar es Salaam
9.        Islamic Culture School – Dar es Salaam
10.    Tanzania Education College – Dar es Salaam
11.    Macmillan Training College – Dar es Salaam
12.    Tanzania International University (TIU) – Dar es Salaam
13.    Dodoma College of Business Management – Dodoma
14.    Faraja Health and Emergencies – Mbeya
15.    St. Joseph College – Mbeya
16.    St. Peter Health Management – Mbeya
17.    Kapombe Nursing School – Mbeya
18.    Uyole Health Institute – Mbeya
19.    Josephine Health Institute – Mbeya
20.    Institute of Public Administration – Chake chake Pemba
21.    Dar es Salaam College of Hotel and Business Studies – Vuga, Unguja, Zanzibar and Chake Chake, Pemba, Zanzibar
22.    Zanzibar Training Institute, the Professional College of Information Technology, Languages and Business Studies – Mwera Meli Sita Unguja  Zanzibar
23.    Azania College of Management – Raha Leo, Zanzibar
24.    Time School of Journalism – Chakechake, Pemba
25.    Residence Professional College – Mombasa, Zanzibar  
26.    Mkolani Foundation Organisation – Mwanza
27.    Kahama College of Health Sciences – Kahama
28.    Institute of Adult Education-Mwanza Campus – Luchelele Site
29.    Zoom Polytechnic – Bukoba
30.    Johrow Star Training College – Shinyanga
31.    St. Thomas Training College – Shinyanga
32.    Dar es Salaam School of Journalism and Mass Communication DMSJ – Bukoba
33.    Dar es Salaam School of Journalism and Mass Communication (DMSJ – Mwanza
34.    Dar es Salaam School of Journalism and Mass Communication (DMSJ – Geita 
35.    Dar es Salaam School of Journalism and Mass Communication (DMSJ – Simiyu
36.    Harvest Institute of Health Sciences – Mwanza
37.    Singin International – Bukoba
38.    College of Business Management – Mombasa, Zanzibar
39.    Tanzania Star Teachers College – Chakechake, Pemba, Zanzibar
40.    Tanzania Star Teachers College – Unguja, Zanzibar
41.    St. Mary’s International School of Business – Sumbawa
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: VYUO 175 NCHINI VYAPEWA NOTISI YA KUSHUSHWA HADHI Rating: 5 Reviewed By: SIMAMA BUKOBA