Kamnda Ras Makunja mkuu wa kikosi kazi ngoma africa band.
Kamnda Ras Makunja mkuu wa kikosi kazi ngoma africa band.
Wanachi Tusikubali kufanywa chambo cha kuvunja amani tuliyoijenga.
Wasanii wa kitanzania wanaoishi na kufanyia kazi zao nje ya
nchi au ughaibuni,wametoa wito kwa wananchi wa Tanzania walio nyumbani na nje kupinga kwa nguvu zote maandamano yaliyopewa na jina la UKUTA
yalipangwa kufanyika siku 1 september 2016. Wasanii hao wakikaliliwa na
na vyombo vya habari walisema maandamano hayo hayana tija kwa
watanzania na zaidi yataleta mpasuko katika jamii. baadhi ya wasanii
hao
ni mwanamuziki Saidi Kanda anayeishi nchi uingerea alisema ”
Hakuna haja ya Kuunga mokono maandamano yatakayo lisababishia taifa
uvunjifu wa amani” baadala yake wanasiasa watuache wananchi tufanye
shughuli zetu na kufurahia maisha- Alisema mwanamuziki Saidi Kanda
kiongozi wa Mvula-Mandondo Band ya Uingereza.
Kule Ujerumani nako Kiongozi wa Ngoma Africa band mwanamuziki
maarufu Kamanda Ras Makunja alikuwa akiongea na vyombo vya habari kwa
niaba ya wasanii waishio ujerumani,mtazamo wa Kamanda Ras Makunja una
hoja nzito kuhusu maandamano ya UKUTA alikaliliwa akisema” Watanzania
tusikubali kufanywa mtaji au chanzo cha vurugu na uvunjivu wa Amani
ambayo kwa miaka tumeijenga,kwani hatuoni sababu yeyote ya msingi ya
kuunga mkono maandamano ya UKUTA, sisi watanzania ndio tuliopiga kura
kuiweka serekali ya awamu ya tano,leo hii
heti tuende mtaani kuandamana kuipinga !? kwa sababu ya watu
wanaojiita UKUTA kwa kweli itakuwa sawa na watoto walio juu ya tawi la
mti na kuanza kulikata tawi walio kalia kwa shoka ni sawa Ukichaa- Ras
Makunja alihoji.
Mwanamuziki huyo nguli alizidi kuhoji hivi wanasiasa si
tuliwapa muda wa kutushawishi kuwapigia kura katika kampeni zao na sasa
uchaguzi umepita
sasa kuna haja gani tena sisi raia
tushawishiwe kuandamana maandamano ambayo tafasiri yake UKUTA kisheria
hayakubaliki ,yaani ukiyatazama kwa upana hayana nia ya AMANI ! yaani
mfano wake yawe maandamano kama yaliyo kuwa IRANI yalioshawishiwa kumtoa
Shah ? lakini Tanzania sio Irani kwa sababu serekali ya Tanzania
imechaguliwa na wananchi kihalali sasa leo sisi wapiga kura tena tuende
mtaani kupinga kitu ambacho tumekichagua kihalali..?
SHAH wa Iran
alikuwa mfalme sio kiongozi wa kuchaguliwa ndio maana Khomen alishawishi
wanafunzi waanze kuandamana, Maandamano ya India 1947 yakiongozwa na
Ghandi yalikuwa ya kumuondoa mkoloni mwingereza,Sasa haya ya UKUTA na
tafisiri yake ipo wazi ni ya nini? kwa faida zipi za taifa
letu,TUNAWAOMBA WANANCHI TUSIKUBALI KABISA KUUNGA MKONO MAANDAMANO YA
UKUTA,tusikubali kushawishiwa kuandamana kwa madai yasiyoleta maandeleo
kwa taifa, tusikubali kila siku baadhi ya wanasiasa wanatuendesha mara
tususie kupiga kura,mara tuandamane UKUTA ,wakati nchi jirani wanachapa
kazi sisi tupo katika siasa kila kukicha ?! Ras Makunja alisisitiza kuwa
anayo haki ya kutoa maoni yake kwani yeye bado raia halali wa Tanzania.
0 comments:
Post a Comment