Waziri wa Elimu,Sayansi na
Teknolojia nchini Tanzania, Prof. Joyce Ndalichako ametoa siku saba kwa
vyuo vikuu vilivyopokea fedha za wanafunzi ambao hawapo vyuoni kwa
mwaka wa 2015/16 kuzirejesha wizarani mara moja.
Taarifa hiyo
ameitoa hii leo jijini Dar es Salaam mbele ya maafisa kutoka wizarani
mwake,pamoja na kaimu mkurugenzi mtendaji wa bodi ya mikopo,na mchunguzi
mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Takukuru na wengineo.
Jumla ya vyuo vya elimu ya juu nchini Tanzania 31 kati ya 81 ndivyo vilivyohakikiwa.Zoezi hilo la uhakiki limefanywa katika awamu tatu kwa kila taasisi ili kuwapa nafasi wanafunzi ambao hawakuweza kujitokeza kwa uhakiki awamu ya kwanza,kujitokeza katika awamu zilizofuata.
0 comments:
Post a Comment