Jeshi la polisi
mkoani Mbeya limesema liko tayari kutoa kibali kwa chama chochote cha
siasa kinachotaka kufanya mikutano ikiwa kitafuata sheria na
taratibu za nchi.
Hayo
yamesemwa na Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya, Dhahiri Kidavashari,
wakati alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari katika Ofisi za
Kituo kikubwa cha Polisi Mkoa wa Mbeya kuhusu matukio mbalimbali ya
kiharifu yaliyotokea.
Amesema
kuwa vibali hivyo vitatolewa kulingana na mazingira ya wakati husika
kwa madai kuwa, hakuna utaratibu wa kufanya mikutano katika Wilaya zote
kwa wakati mmoja.
Amesema
kuwa kwa mujibu wa Sheria, mikutano hiyo inahitaji ulinzi wa polisi kwa
ajili ya kulinda amani, hivyo akasema kuwa lazima vibali hivyo
vizingatie hali ya wakati huo.
“Haiwezekani
tukaruhusu maandamano katika Wilaya zote maana maandamano na mikutano
hiyo inahitaji ulinzi wa Jeshi la Polisi, sasa tukiruhusu vitu kama
hivyo tutashindwa kuweka ulinzi katika mikutano hiyo, kwa hiyo
tutaangalia mtu atakayefuata taratibu ndiye atakayeruhusiwa na kupewa
ulinzi,” alisema Kidavashari.
Amesema
kuwa yeyote atakayeomba kibali kwa mujibu wa taratibu ndiye atakaye
pewa ulinzi, lakini atakayekiuka atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
Aliwataka wananchi
kutokubali kurubuniwa na wanasiasa ili kushiriki katika maandamano
yaliyokatazwa kwa madai kuwa watashughulikiwa na jeshi hilo kwa mujibu
sheria zinavyotaka jeshi hilo kufanya.
Aliwataka
kuwa na uhakika na mikutano wanayohudhuria endapo inakuwa imeruhusiwa
ama la, ili wasijewakajikuta wanajiingiza katika matatizo.
Siku
za hivi karibuni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
kilitangaza kuwa kufikia Septemba mosi mwaka huu kitafanya maandamano
nchi nzima ili kupinga kile walichokiita udikteta ambayo waliyabatiza
jina la Ukuta.
0 comments:
Post a Comment