TANGOZO

TANGOZO
Latest News
Thursday, September 15, 2016

Kinywaji cha ''kupoteza ubikira'' chazua mjadala China


Kinywaji maarufu kwa jina ''blackout in a can' nchini Marekani kimeingia nchini China.

Four Loko ,kinywaji kilicho na ladha ya matunda na asilimia 12 ya pombe kilitumika sana katika sherehe nchini Marekani kabla ya kuondolewa madukani katika majimbo kadhaa hadi pale viungo vyake viliporekebishwa.

Na sasa kimepata umaarufu mkubwa nchini China ,huku raia wakikiita ''Lose Virginity'' {poteza ubikira}kwa kuwa wanahisi kinywaji hicho kina nguvu zaidi.


Wanavlogu kadhaa wamepakia kanda za video wakinywa kinywaji hicho cha mililita 695.

Kinywaji hicho kiligonga vichwa vya habari hivi majuzi baada ya wanawake watatu walio katika umri wa miaka 20 kuficha na kuingiza kinywaji hicho katika baa moja ya karaoke,kupoteza fahamu baada ya kunywa na kupoteza vitu vyao vyote kwa wezi..

  • Je, Four Loko ni nini haswa ,na watu wanasema nini kuhusu kinywaji hiki?
Four Loko kimeelezewa katika mitandao ya kijamii nchini China kuwa kinywaji kilicho na pombe pamoja na kafeini.

Baadhi ya watu wanadai kwamba mchanganyiko huo unakifanya kinywaji hicho kuwa na nguvu na kina uwezo wa kumfanya mtu kupoteza fahamu baada ya kunywa chupa moja tu
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: Kinywaji cha ''kupoteza ubikira'' chazua mjadala China Rating: 5 Reviewed By: SIMAMA BUKOBA