TANGOZO

TANGOZO
Latest News
Monday, July 18, 2016

AGIZO LA RAIS MAGUFULI KWA VIONGOZI WA JESHI LA POLISI

July 18 2016 Naibu Makamishna wa Polisi 25 na Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi 35 wamekula kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma, Ikulu Jijini Dar es salaam.

Muda mfupi baada ya kiapo hicho Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaagiza viongozi wa Jeshi la Polisi Tanzania kuwaondoa watumishi wote wasiokuwa askari polisi na ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya ukiukwaji wa taratibu na ufujaji wa fedha za umma ili kulinda heshima, nidhamu na uadilifu ndani ya jeshi hilo, Rais Magufuli amesema.

Mnajua kupeleleza, mna vyombo vyote, ofisi ya IGP (Inspekta Jenerali wa Polisi) ipo palepale, ofisi ya DCI (Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai) ipo palepale, Makamishna wote mnazunguka mnakwenda palepale, mwizi mnae palepale, mnashindwa kumshika.

”Kama mnafikiri kuwa na raia katika jeshi la polisi wanawaharibia kazi zenu hamisheni raia wote na wapelekeni utumishi, kwani hakuna mhasibu ambaye ni askari polisi? hakuna mhandisi ambaye ni askari polisi? hakuna afisa tawala ambaye ni askari polisi?’
 
‘Mimi nafikiri kama matatizo ya wizi na wafanyakazi hewa yanaletwa na raia waliomo ndani ya jeshi la polisi na majeshi yetu mengine, IGP kaorodheshe raia wote wanafanya kazi Jeshi la Polisi ili waondolewe na tuwapangie kazi nyingine uraiani’

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: AGIZO LA RAIS MAGUFULI KWA VIONGOZI WA JESHI LA POLISI Rating: 5 Reviewed By: SIMAMA BUKOBA